Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji, amejitokeza hadharani na kutoa maagizo mazito kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo, ambapo amewataka kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja ujenzi wa uzio uwe umekamilika ili waachane na matumizi ya viwanja vya kukodi.
Wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Uwanja wa Mo Simba Arena huko Bunju, mwaka 2020, Mo Dewji aliahidi mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa wakati huo, Dk Harrison Mwakyembe kuwa atatoa gaharama zote za ujenzi wa awali za uwanja huo jambo ambalo alifanikisha.
Akizungumza katika ziara ya ujenzi huo, Bunju jijini Dar es Salaam, Mo alisema kwamba, anajisikia aibu kuona klabu kubwa kama Simba inaendelea kufanya mazoezi kwenye viwanja vya kukodi hivyo akaagiza ujenzi wa uzio uishe mara moja.
Dejan: Mkataba wangu umevunjwa Simba SC
“Natumaini ujenzi wa uzio huu utakamilika ndani ya miezi mitatu na kwamba, kufikia mwakani tutakuwa na uhakika wa kuutumia katika baadhi ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara, hivyo nawaomba sana viongozi wenzangu mhakikishe mnasimamia ujenzi ili umalizike kwa wakati,” alisema Mo.
Kwa Upande wa Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema: “Kweli Rais wa Heshima Mo, ametoa maagizo ya kumalizika haraka kwa ujenzi wa uzio na kwamba mipango yake ni mikubwa sana juu ya ujenzi huo, ila habari njema ni kwamba uwanja unaenda kukamilika ndani ya mwezi mmoja tu tayari timu itaanza kufanya shughuli zake.”