Jarida maarufu Duniani la Forbes limetoa orodha mpya ya mabilionea 18 wanaoongoza kwa utajiri barani Afrika, huku kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida hilo utajiri wao wote kwa ujumla ukiwa dola bilioni 74.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa Aprili 6, 2021, Aliko Dangote wa Nigeria anaendelea kuongoza kwa utajiri kwa mwaka wa 10 mfululizo huku utajiri wake ukiwa dola bilioni 11.6. Hata hivyo, Dangote ni wa 190 katika orodha ya matajiri wa dunia nzima.

Barani Afrika, Dangote alifuatwa na Nassef Sawiris wa Misri utajiri wake ukiwa ni dola bilioni 8.5, Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini akiwa na utajiri wa dola bilioni 8, Johann Rupert wa Afrika Kusini akiwa na dola bilioni 7.2 huku Mike Adenuga wa Nigeria thamani yake ikiwa ni dola bilioni 6.3.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Mtanzania Mohammed Dewji pekee ndiye aliyeingia katika orodha hiyo.

Ingawa idadi ya matajiri hao katika jarida la Forbes iliongezeka kote duniani huku ikiweka rekodi kwa kuongeza watu wapya 493, idadi ya mabilionea wa Afrika ilipungua kidogo ikilinganishwa na mwaka 2020 ilipokuwa 20.

Mabilionea 18 wa Afrika wanatoka mataifa mbalimbali kama vile Afrika Kusini na Misri zikiwa na matajiri watano kila mmoja, Nigeria ikiwa na matajiri watatu, Morocco matajiri wawili, Zimbambwe, Tanzania na Algeria wakiwa na tajiri mmoja kila mmoja.

Orodha kamili ya mabilionea wa Afrika kwa mujibu wa Forbes:

1. Aliko Dangote – Nigeria – ana thamani ya $11.6b

2. Nassef Sawiris – Misri – ana thamani ya $8.5b

3. Nicky Oppenheimer – Afrika Kusini – thamani ya $8b

4. Johann Rupert – Afrika Kusini – ana thamani ya $7.2b

5. Mike Adenuga – Nigeria – ana thamani ya $6.3b

6. Abdulsamad Rabiu – Nigeria – ana thamani ya $ 5.5b

7. Issad Rebrad – Algeria – ana thamani ya $4.8b

8. Naguib Sawiris – Misri – ana thamani ya $3.2b

9. Patrice Motsepe – Afrika Kusini – ana thamani ya $ 3b

10. Koos Bekker – Afrika Kusini – ana thamani ya $2.8b

11. Mohamed Mansour – Misri – $2.5b

12. Aziz Akhannouch – Morocco – $2.0b

13. Mohammed Dewji – Tanzania – $1.6b

14. Youssef Mansour – Misri – $1.5b

15. Othman Benjeloun – Morocco – $1.3b

16. Michiel Le Roux – Afrika Kusini – $1.2b

17. Strive Masiyiwa – Zimbabwe – $ 1.2 b

18. Yaseen Mansour – Misri – $1.1b

Billioni 1.5 kuwanufaisha wasanii
Mtibwa Sugar: Hitimana bado mali yetu