Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amemteua Bilionea na Mfanyabiashara wa Tanzania, Mohammed Dewji, kama mmoja wa washauri wake wa maswala ya uwekezaji.

Moo Dewji maarufu kama ‘MO’, ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), atakaa kwenye baraza la ushauri la uwekezaji la Rais Ramaphosa, kwa kipindi cha miaka mitatu.

Wakati huohuo, Jarida maarufu la Forbes hivi karibuni limetoa orodha ya Mabilionea 18 barani Afrika huku Mo Dewji akiwa Bilionea pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki aliyeingia katika orodha hiyo.

Mtibwa Sugar: Hitimana bado mali yetu
KMC FC yatuma salamu Young Africans