Rais wa Heshima wa Simba SC Mohammed Dewji ‘MO’ amesema hana kinyongo na aliyekuwa Afisa Habari wa Klabu hiyo Haji Sunday Manara, licha ya kumtolewa maneno machafu tangu alipoondoka klabuni hapo miaka miwili iliyopita.

Manara aliondolewa Simba SC kwa tuhuma za kimaadili ambazo hazithibitisha na uongozi wa klabu hiyo hadi sasa, lakini mtuhumiwa bila uwoga aliwahi kuzizungumza tuhuma hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari siku chache baada ya kuondoka Msimbazi.

Mo Dewji ambaye pia ni Mwekezaji Mwenza wa Simba SC, amedai kuwa Manara amekuwa akimtukana, na anaendelea kufanya hivyo mara kwa mara, lakini yeye hana kinyongo naye na kubainisha kuwa amemsamehe na kwamba amemwachia Mungu.

“Turudi kwa huyu ndugu yetu, tumefanya naye kazi vizuri, najua kwamba alikuwa amenitukana na anaendelea kunitukana.”

“Lakini Mimi nimemsamehe, kwani maisha ni mafupi, yamepita hata kama akiendelea kunitukana Mimi namsamehe na sio yeye kuna wengine pia ambao wamenisema vibaya na kunitukana.”

“Mimi ni aina ya mtu ambaye siweki chuki ndani ya moyo wangu. Mungu amenijalia vitu viwili, kwanza sina wivu na mtu, pili sibaki na kinyongo, maana yake ikitokea jambo Mimi nasamehe, namuachia mwenyezi” amesema MO kwenye sehemu ya mahojiano yake kuhusu klabu hiyo.

Haji Manara kwa sasa ni sehemu ya watumishi wa Young Africans akihudumu katika Idara ya Habari na Mawasilino inayoongozwa na Ally Kamwe.

Victor Akpan amkingia kifua Fei Toto
Meridianbet Kasino ya Mtandaoni Ushindi kila dakika