Mshambuliaji kutoka Misri na Klabu ya Liverpool, Mohamed Salah anataka kuweka rekodi baada ya bao lingine la kihistoria kuipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Brentford, kwenye Ligi Kuu, Jumamosi (Mei 06).
Salah alifunga bao hilo dakika ya 13 likiwa la 30 msimu huu ikiwa ni mara ya nne kufikisha idadi hiyo ya mabao na bao lake la 100 akiwa Anfield yalipo makao makuu ya klabu yake ya Liverpool.
Alikuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga katika mechi tisa mfululizo za nyumbani na kwa kufanya hivyo alifikia rekodi ya Steven Gerrard katika nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu akiwa na mabao 186.
“Ina maana kubwa kwangu. Nilisema hapo awali, ninahisi (niko) nyumbani hapa, nina furaha,” alisema Salah akiambia Sky Sports.
“Ni kitu ambacho kinanifanya nijivunie, kuwa mwadilifu. Ninafanya kazi kwa bidii na kila mtu anajua hilo, kila mtu analiona hilo.
“Nimehamasishwa tu kuweka rekodi na kufunga mabao na michezo ya ushindi kwa timu.”
Kwa upande wa Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alitoa sifa nyingi kwa kuhusu ubora wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
“Namba anazotengeneza, sote tunajua kwamba baada ya kazi yake ataonekana kama mmoja wa magwiji wa wakati wote, hiyo ni wazi,” alisema bosi huyo wa Wekundu hao.
“Lakini sasa bado yuko kwenye kazi na watu wengine wanaweza kutomthamini vya kutosha, lakini tunafanya hivyo.