Hatimaye Uongozi wa Azam FC umemtangaza Kocha Abdi Hamid Moallin kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Azam FC imemtangaza Kocha huyo kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Somalia leo Jumanne (Januari 25), jijini Dar es salaam.
Kocha Moallin alipewa jukumu la kukiongoza kikosi cha Azam FC kama kocha wa muda, baada ya kuondoka kwa George Lwandamina mwishoni mwa mwaka 2021.
Tangu alipokabidhiwa kikosi cha Azam FC, Kocha Moallin alionesha uwezo mkubwa kwa kuleta mabadiliko kwenye kikosi cha klabu hiyo, huku akifika Fainali ya Kombe la Mapinduzi, na kupoteza dhidi ya Simba SC.
Upande wa Ligi Kuu amepoteza mchezo mmoja dhidi ya Simba SC, kwa kufungwa mabao 2-1, Januari Mosi 2022, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Awali Moallin aliajiriwa klabuni hapo kama Mkurugenzi wa Ufundi wa Maendeleo ya Soka la Vijana.