Aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Al Ahly na Misri, Mohamed Aboutrika ameongezwa kwenye orodha ya magaidi nchini humo kufuatia kutuhumiwa kuwa na uhusiano na kikundi cha Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku.

Aboutrika anatuhumiwa kukifadhili kikundi cha Brotherhood kinachotafsiriwa kama kundi la kigaidi nchini Misri.

Katika uchaguzi wa mwaka 2012, Aboutrika alimpendekeza mgombea wa Brotherhood, Mohamed Morsi ambaye alishinda  urais na kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kung’olewa madarakani na kuorodheshwa kwenye orodha ya magaidi nchini humo.

Aboutrika pia amekuwa akiunga mkono nchi ya Palestina na kuvaa fulana za kuwaunga mkono raia wa nchi hio katika vuguvugu dhidi ya Israel.

Wakili wa Aboutrika, Mohamed Osman amesema Aboutrika ameorodheshwa kama gaidi licha ya kutofikishwa mahakamani wala kujulishwa kutuhumiwa.

” Tutakataa rufaa kupinga haya maamuzi,” Amenukuliwa Osman huku Aboutrika mwenyewe akikana tuhuma hizo.

Yaya Toure Akataa Mshahara Mnono
Ndege ya Jeshi la Nigeria yashambulia kambi ya wakimbizi kimakosa