Hatimae uongozi wa klabu ya Simba umemuandikia barua mfanyabiashara (Bilionea) Mohamed Dewji “Mo”, ya kumktaka ahudhuria kwenye kikao maluum cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ili kueleza dhamira yake ya kutaka kuwekeza kiasi cha shilingi billioni 20.

Katibu mkuu wa  klabu ya Simba Patrick Kahemele, amemuandikia “Mo” barua hiyo, kwa kumthibitishia maazimio yaliyopitishwa na wanachama katika mkutano mkuu wa klabu ya Simba ambao ulifanyika jana katika ukumbi wa bwalo la polisi jijini Dar es salaam.

Katika barua hiyo “Mo” ameombwa kukutana na kamati ya utendaji ya klabu ya Simba Agust 15 mwaka huu.

Lembeli achungulia CCM, Magufuli aahidi kutomkata 'mkia' akirudi
Video: 'Serikali yangu haihitaji kodi za watu wanyonge' - Magufuli