Siku moja baada ya mkutano mkuu wa Simba kumalizika kwa kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu hio, mfanyabiashara (bilionea) Mohamed Dewji ameibuka na kuwashukuru wanachama wa Simba kwa uamuzi huo na kupinga hoja ya kuwa hajazungumza na viongozi wa klabu hio.

Katika mkutano mfupi na waandishi alioufanya mapema hii leo ofisi kwake jijini Dar es salaam, Dewji alianza kwa kuwashukuru wanachama wa Simba kwa kupitisha ajenda ya mabadiliko licha ya viongozi kutowasilisha taarifa ya maoni ya kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji.

“Mimi Mohamed Dewji nawashukuru sana wanachama wa Simba kwani wamevuja damu, jasho kwa ajili ya Simba, nasema nitakuwa nao bega kwa bega.”

“Kwa namna moja au nyingine, kuna hoja zimeniumiza na zilikuwa za upotoshaji na nimeona ni vyema kuziongelea kwa undani.”

“Kuna hoja ya kwanza viongozi wanasema natangaza kwenye vyombo vya habari na sisi hatujawahi kukutana. Leo labda niwe wazi zaidi, nishakutana na Rais wa Simba, Evan Aveva zaidi ya mara tatu. Alikuja na wajumbe wa kamati kuu.”

Dewji pia amefafanua hoja ya kutotuma ofa yake kwa maandishi na kudai alikuwa anasubiria ridhaa ya wanachama. Kwa kuwa wanachama wameshatoa ridhaa ametuma rasmi barua kwa viongozi wa Simba.

“Leo asubuhi nimeandika barua kwenda kwa Rais wa Simba bahati mbaya ofisi yake imefungwa, ikifunguliwa tu barua yangu ya kwanza”.

” Ni dhahiri kwamba baadhi ya viongozi wanaoongozwa na Rais Evans Aveva hawataki mabadiliko lakini nashukuru wanachama wananiunga mkono”.

Lowassa Adai Angeanza Kushughulika na Maslahi ya Waalimu na Siyo Madawati
Mnangagwa akanusha madai kupindua Serikali ya Mugabe