Aliyekuwa Waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Somalia baada ya aliyekuwa Rais, Hassan Sheikh Mohamud kukubali kushindwa katika uchaguzi, ambapo Farmajo alipata kura 184 na Hassan Sheikh akipata kura 97 naye Rais mwingine wa zamani Sharif Sheikh Ahmed akapata kura 46.

Farmajo alikuwa waziri mkuu nchini Somalia mwaka 2010 na 2011.

Farmajo wakati akiongea na wabunge waliokusanyika katika ukumbi ulio katika uwanja wa ndege Mogadishu, ambao ndio waliomchagua amesema kuwa ushindi huo ni wa Somalia na kwa Wasomali,”.

Aliapishwa kura rais muda mfupi baadaye.

Taifa la Somalia linalokabiliwa na vita vya kikabila pamoja na vile vya ukoo halijafanikiwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia unaoshirikisha raia kushiriki katika uchaguzi tangu 1969.

 

Dimitri Payet, Memphis Depay Wafanya Yao Ufaransa
JPM amtumbua katibu tume ya mipango wizara ya fedha