Hatimae klabu ya Arsenal, imekamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Misri na klabu ya FC Basel ya nchini Uswiz, Mohamed Naser Elsayed Elneny.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alithibitisha taarifa za kusajiliwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, usiku wa kuamkia hii leo, dakika chache baada ya mchezo wa ligi ya England kumalizika dhidi ya Liverpool.

Tayari imeshaanza kuhisiwa huenda Elneny, akawa sehemu ya kikosi cha Arsenal, katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo The Gunners watafunga safari kuelekea Stoke On Trent kupambana na Stoke City.

“Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.” Alisema Wenger

Elneny, anaripotiwa kuigharimu Arsenal kiasi cha paund million tano ambacho ni ada yake ya usajili.

Rekodi Mpya: Mtu Mzee zaidi Duniani abainika, Fahamu umri na maisha yake
Ligi Ya England Inaendelea Kustaajabisha