Shirikisho la soka la Misri ‘EFA’ litampa mapumziko ya juma moja Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na hatacheza mechi inayofuata ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2023).

Salah alijumuishwa na kocha Rui Victoria katika kikosi kitakachocheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Ethiopia, lakini staa huyo ameambiwa atapewa muda wa kupumzika na ataripoti kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Tunisia itakayochezwa Septemba 12.

Uamuzi huo umetolewa baada ya Liverpool kugomea ofa ya Pauni 200 milioni iliyowasilishwa na Al-Ittihad kwa ajili ya kutaka kumsajili mkali huyo, kwani majogoo hao hawana mpango wa kumuuza Salah katika dirisha la usajili la kiangazi lililofungwa rasmi Septemba mosi.

Awali, timu hiyo kutoka Saudi Arabia ilituma ofa ya Pauni 150 milioni lakini Liverpool ikaipotezea.

Hata hivyo, mambo yanaweza kubadilika endapo Salah atalazimisha kuondoka kwa sababu dirisha la usajili bado lipo wazi kule Saudia.

Mashabiki wa Liverpool waliamini kwamba Salah angeondoka kutokana na ofa kubwa iliyoandaliwa na Waaralbu, lakini uhamisho huo ukagonga mwamba.

Juma lililopita mkongwe wa Liverpool, Robbie Fowler aliwaonya mashabiki wa Livperpool kuwa Mohamed Salah anaweza kuondoka Anfield.

Fowler anayefundisha katika Ligi Daraja la Pili Saudi Arabia alikiri kwamba hatashangaa endapo Salah ataamua kuondoka.

ATCL kumiliki Ndege B737 mpya Septemba
Kampuni yakanusha umiliki ekari Mil. 6 eneo la Hifadhi