Taasisi ya Mifupa (MOI) imefanikisha kufanya upasuaji mkubwa wa kurudisha ubongo wa mtoto wa miezi minne ndani ya kichwa baada ya mtoto huyo kuzaliwa huku ubongo wake ukiwa kwenye mfuko nje ya kichwa.

Upasuaji huo wa kipekee umefanywa kwa zaidi ya masaa manne na jopo la Madaktari bingwa wa ubongo na mgongo, wakiongozwa na Dkt. Nicephorus Rutabasibwa ambao wote kwa pamoja ndani ya kipindi cha miezi miwili walikuwa wakitafiti namna bora ya kumfanyia upasuaji mtoto huyo.

Aidha kutokana na tafiti hizo ilionekana kuwa mtoto huyo alizaliwa na uvimbe ambao ulikuwa umefunika sehemu kubwa ya ubongo na mishipa ya damu hali ambayo ingehatarisha maisha na ukuaji wake kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi ya Moi imesema kuwa Madaktari hao wamekumbwa na changamoto kadhaa wakati wanatekeleza jukumu hilo la upasuaji ikiwa ni pamoja na mishipa midogo ya mtoto huyo ambayo imepelekea asiliimia kubwa ya ubongo wake kuwa kwenye uvimbe.

Hata hivyo, inasemekana kuwa upasuaji huo wa kipekee umefanikiwa baada ya kuwepo na vifaa vya kisasa kwenye chumba cha upasuaji MOI pamoja na umahiri wa madaktari.

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 6, 2017
Video: Majeshi ya Umoja wa Afrika Mashariki kujifua kwa siku 17