Kampuni ya EAA Co. ltd ya nchini Japan imetoa msaada wa viungo bandia vyenye thamani ya shilingi milioni 80.9 kwa Taasisi ya Tiba  ya Mifupa (MOI) leo Aprili Mosi 2020, jijini Dar es Salaam.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa tiba MOI Dkt Samwel Swai amesema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa matibabu ya wagonjwa wenye ulemavu wa miguu na mikono.

Naye meneja wa kampuni ya EAA C.o Ltd Josiah Benedict amesema ameguswa na changamoto zinazowakabili watanzania ndiyo maana wameamua kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt Pombe Magufuli yakuboresha huduma ya afya hapa nchini.

Aidha msaada huyo unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania na Japan kwa kushirikiana na watanzania waishio nchini humo.

 

Wagonjwa wa Corona waongezeka Tanzania wafikia 20
Ajax yaachana na Abdelhak Nouri