Mwanasiasa maarufu wa chama cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Moise Katumbi amewasili katika mji wa Kasumbalesa ulioko mpakani baada ya serikali ya Kinshasa kumkatalia kuingia nchini humo.
Awali Katumbi alikuwa na nia ya kuingia kwa ndege katika mji wa Lumbumbashi lakini alilazimika kutua katika mji wa Ndola Zambia na kusafiri kwa gari hadi mji wa Kasumbalesa ambako amepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Kongo.
Kiongozi huyo wa upinzani anarudi nchini ili kujiandikisha kushiriki kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa urais Disemba 2018, kwani siku ya mwisho kujiandikisha ni Agosti 8.
Aidha, Mwanasiasa mwingine mashuhuri wa upinzani Jean Pierre Bemba aliwasili Kinshasa siku ya Jumatano baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 11 na alijiandikisha kama mgombea kiti cha rais.
-
Jinsi ya kufanya kazi na Bosi msumbufu
-
Mama yake Osama anena kwa mara ya kwanza kuhusu mwanaye
-
Mama yake Osama anena kwa mara ya kwanza kuhusu mwanaye
Hata hivyo, Katumbi ambaye alikuwa Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ambaye pia ni mfanyabiashara tajiri, alilazimika kwenda uhamishoni tangu Mei 2016 baada ya uhusiano wake na Rais Joseph Kabila kuharibika na kuhukumiwa na mahakama kwa kujaribu kuvuruga usalama wa taifa