Imefahamika kuwa Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umemalizana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini DR Congo Jesus Moloko kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya ule wa miaka miwili kumalizika.

Young Africans imempa Moloko mkataba wa mwaka mmoja ambao ni sawa na ule alioutumikia Nabi kwa mara ya mwisho ambao ulimalizika pia mwisho wa msimu huu kisha akagoma kuongeza mwingine.

“Tumeona tumpe mkataba mpya ni winga ambaye ameonyesha kiwango bora hasa msimu huu, tutampa nafasi ya kumuangalia katika mwaka mwingine kama ataendeleza kasi yake,” amesema bosi mmoja wa juu wa Young Africans.

Moloko ambaye aliimarika zaidi msimu huu amesaini mkataba huo akishinda vita ya awali kupigiwa hesabu za kusitishiwa mkataba wakati akimaliza mwaka wa kwanza.

Young Africans ilipiga hesabu za kumtoa kwa mkopo Singida Big Stars wakati alipoona kiwango bora cha winga Mbrazil, Frederico Dario ambaye hata hivyo baadae alitimka klabuni hapo akirejea kwao.

Baada ya hesabu hizo ilikuwa ni kama zimemshtua Moloko ambaye alirudisha makali yake na kuifanya Young Africans kumvuta mezani.

Vyama vishirikiane kuiondoa CCM madarakani - Bulaya
Picha: Rais Samia katika uapisho Ikulu Dodoma