Muigizaji maarufu wa bongo movie Vyonne Cherry ‘Monalisa’, anatarajia kuzindua mpango kazi ‘program’ ya kuinua vipaji vya wasichana wapya kwa ajili ya uigizaji inayojulikana kama ‘Act with Monalisa’

Muigizaji huyo ambaye tayari  amekuwa  akifanya mchakato mbalimbali kwa kuagali vipaji vipya kupitia program hiyo amabyo anatarajiwa kuizindua rasmi tayari ameshaanza kukutana na wasichana mbalilmbali.

Amesema kuwa mpango kazi huo ni kwaajili ya mwaka 2019 na 2020 ili kupata vipaji vipya kwa watoto wa kike ambapo watashindana wao kwa wao na kupata waigizaji wazuri na bora zaidi.

”Tutazindua rasmi mpangokazi huu kwa mwaka huu mapema mwezi ujao endelea kufuatilia kurasa wetu za mitandao ya kijamii,”  instagram @ monalisatz.alisema.

 

 

Watalii zaidi ya 1000 kuzuru nchini
Bondia ageuka kuwa muuaji katili zaidi Marekani