Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Justine Monko amesema kuwa kauli aliyoitoa Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Lazaro Nyalandu kuwa CHADEMA inaenda kushinda majimbo yote ndani ya Mkoa wa Singida na kudai kuwa jambo hilo halitawezekana kwasasa.
Mbunge huyo wa Singida Kaskazini amesema kauli aliyoitoa hivi karibuni, ni kauli ya kisiasa bali anachojua yeye majimbo yote ya mkoa huo kwenye Uchaguzi Mkuu 2020, majimbo hayo yatabaki CCM.
“Kuhusiana na kauli ya Nyalandu sidhani kama kuna lolote, kwa sababu ni kauli ya mwanasiasa yeyote, huwezi kusema hautashinda, sasa kwa vile karudi kivingine kupitia CHADEMA lazima awaaminishe watu wanaenda kushinda japo sijajua amejipangaje kufikia mahali pa kushinda majimbo yote ya Singida, ila nachojua Mkoa wa Singida bado unapendwa sana na wananchi.” amesema Justine Monko.
Amesema kuwa yeye anachojua majimbo yote ya Mkoa wa Singida yatabaki CCM kwa sababu kuna kazi wamezifanya, ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiasi kikubwa, na hilo ndilo litakalowafanya washinde.
Hivi karibuni akiwa mkoani Singida kwenye kampeni ya CHADEMA ni msingi, Lazaro Nyalandu alisema kupitia watu maarufu wa mkoa huo akiwemo yeye pamoja na Tundu Lissu watahakikisha wanashinda majimbo yote manne ya mkoa huo.
-
Monko amjibu Nyalandu, ‘CCM iko imara sana’
-
HESLB yatoa mwongozo kwa waombaji mkopo elimu ya juu 2019/2020
-
Serikali ya Awamu hii ya Tano inamsimamo kweli- Zitto Kabwe