Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa morali ya kufanya kazi ya kibunge imepungua kwakuwa bunge limekosa hadhi ya kutoa maamuzi.

Godbless Lema ndiye aliyekuwa Mbunge wa kwanza kulalamikiwa kupitia ofisi ya Spika, wakati mkutano wa 13 wa vikao vya Bunge la Tanzania ambapo Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaja Mbunge huyo kwenye orodha ya wabunge wenye mahudhurio hafifu ndani ya bunge pamoja na kamati anazoshiriki.

Kwenye kikao hicho kilichofanyika mwezi Novemba 2018, Spika Job Ndugai alisema Mbunge Lema ana mahudhurio yasiyoridhisha, kuliko wabunge wengine na akifika bungeni mbunge huyo amekuwa hamalizi vikao vyote vya siku.

“kwangu mimi bunge limepoteza hadhi sio maamuzi ya wabunge yanayoweza kusababisha mabadiliko ya taifa hili, kwa maana hiyo morali ya kufanya kazi ya kibunge ndani ya bunge inapungua na badala yake inatulazimu kujenga wigo mpana nje ya bunge, ili inapokuja uchaguzi wa 2020 tuwaondoe wabunge wa CCM.”alijibu Lema

Hata hivyo, Sakata la utoro halikuishia kwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, pia jana lilimkumba Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari baada ya kutajwa na Mbunge wa viti maalum wa CCM, Amina Mollel kuwa mbunge huyo haonekanai Bungeni.

 

Manaibu waziri wasisitiza usimamizi mzuri wa Wakandarasi
Dkt. Bashiru awawashia moto ‘wanaokamuana’ mitandaoni