Ikiwa tayari imeshawasajili wachezaji wanne tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Agosti Mosi, tetesi zinaeleza kuwa klabu ya Young Africans huenda ikawatema wachezaji zaidi ya 10, ili kutoa nafasi kwa wachezaji wanaotarajiwa kuleta mabadiliko kuanzia msimu wa 2020/21.

Tetesi hizo zinaeleza kuwa wachezaji watakaoachwa klabuni hapo, wanakabiliwa na sababu kadhaa ikiwemo ya utovu wa nidhamu pamoja na kushuka kwa viwango, huku wengine mikataba yao ikifikia ukingoni.

Wachezjai wanaotajwa huenda wakatemwa na Young Africans ni

1. Benard Morissonâž¡ Nidhamu mbovu

2. Papy Tshishimbiâž¡Nidhamu pia mkataba umeisha

3. Kelvin Youndanâž¡Nidhamu mbovu

4. Japhary Mohamedâž¡Kiwango duni

5. Raphael Daudâž¡Kiwango duni

6. David Molingaâž¡Nidhamu mbovu

7. Ally Allyâž¡Kiwango duni

8. Ally Mtoni Sonsoâž¡Kiwango duni

9. Andrew Vicent Danteâž¡Kiwango duni

10. Sospeterâž¡Kiwango duni

11. Adam Kiondoâž¡Kiwango duni

12. Tariq Seifu Kiakalaâž¡Kiwango duni

13. Juma Mahadhiâž¡Kiwango duni

14. Paul Geofrey Boxerâž¡Kiwango duni

15. Foruck Shikaloâž¡Kiwango duni

16. Yikpeâž¡Kiwango duni

17. Erick Kabambaâž¡Kiwango duni

18. Adeyum Salehâž¡Kiwango duni

19. Gustavo Simonâž¡Kiwango duni

20. Mohamed Bankaâž¡Nidhamu pia mkataba umeisha

Wachezaji waliosajiliwa na Young Africans hadi sasa ni Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo akitokea Mbao FC walioporomoja Daraja, kwa kufungwa na IHEFU FC kwenye mchezo wa mtoano, mwishoni mwa juma lililopita.

Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar, Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini  Mustapha wa Polisi Tanzania FC.

Fedha za FIFA kunufaisha mikoa Tanzania Bara, Zanzibar
Makonda'' nimekamilisha safari yangu ya ukuu wa mkoa''