Kocha wa muda wa kikosi cha timu ya taifa ya Uganda Moses Basena ameungana na kocha wa timu ya taifa ya Togo Claude LeRoy, katika harakati za kusaka kibarua cha kukinoa kikosi cha The Cranes.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Uganda FUFA imeeleza kuwa, mpaka sasa makocha zaidi ya 200 wametuma maombi ya kutaka kuajiriwa, baada ya nafasi hiyo kutangazwa siku kadhaa zilizopita.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ya ukuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uganda, ni Novemba 15 mwaka huu.

Basena ameeleza sababu ya kuwa miongoni mwa waliomba kazi ya kutaka kuwa kocha mkuu wa Uganda, kwa kuamini muda wa kufanya hivyo umefika baada ya kuwa msaidizi kwa kipindi kirefu.

Basena, ambaye aliwahi kuzifundisha baadhi ya klabu za nchini Uganda, amekua kocha wa muda wa kikosi cha Uganda tangu alipoondoka Milutin ‘Micho’ Sredojevic miezi miwili iliyopita.

“Nimefanya kazi kama msaidizi kwa kipindi kirefu, na sasa nimeamua kuomba nafasi ya kuwa kocha mkuu kwa jili ya kulisaidia taifa langu kufaniisha safari ya kufuzu fainali za Afrika za 2017,” Basena ameliambia shirika la utangazai la Uingereza BBC.

Katika utawala wa Micho, Basena alionyesha kufanya kazi kwa ukaribu na kocha huyo mzaliwa na Serbia, na kuchangia mafanikio ya kuiwezesha The Cranes kufuzu fainali za Afrika za 2017 zilizochezwa nchini Gabon.

Pia aliisaidia kuifikisha Uganda katika fainali za mataifa bingwa (CHAN) zitakazofanyika mwaka 2018.

Akiwa katika majukumu ya kocha wa muda, Basena tayari ameshakiongoza kikosi cha Uganda katika mchezo dhidi ya Misri ambao ulimalizika kwa The Cranes kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri mjini Kampala, kabla ya kwenda mjini Cairo na kupoteza mchezo wa pili wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Mwingine alieomba nafasi ya kutaka kuwa kocha mkuu wa Uganda ni kocha Joao Miguel de Castro Ferreira kutoka nchini Ureno, ambaye anatambuliwa na shiriisho la soka barani Ulaya UEFA.

Kiongozi huyu wa upinzani ahukumiwa jela miaka 25
Kenyatta awataka NASA kwenda mahakamani