Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Chelsea Victor Moses, anatarajia kukamilisha usajili wa mkopo kwa kujiunga na wagonga nyundo wa jijini London, West Ham Utd kabla ya dirisha la usajili kufungwa hii leo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, analazimika kufanya mikakati ya kuelekea upande wa pili huko magharibi mwa jijini London, baada ya masuala kumuendea kombo kwa kukosa kucheza kila juma chini ya meneja Jose Mourinho.

Hii itakua ni mara ya tatu kwa Moses kuondoka Chelsea kwa mkopo kwa sababu za kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hali ambayo inatoa msukumo wa kukaribia kuuzwa moja kwa moja kwenye klabu itakayokua tayari kumsajili.

Moses aliwahi kuuzwa kwa mkopo kwenye klabu ya Liverpool na Stoke City, na alipokua na vikosi vya klabu hizo alikua akicheza mara kwa mara.

Mkataba wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, na klabu ya Chelsea, bado umesaliwa na muda wa miaka miwili.

Victor Moses alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2012, kwa ada ya paund million 9, akitokea kwenye klabu ya Wigan Athletic.

De Gea Mashakani Kurejea Nyumbani
Sitta Adai Wanaweza Kumshtaki Lowassa, Lowassa Awataka Wananchi Wasiogope