Mshambuliaji kutoka Zambia Moses Phiri amesema hajawahi kucheza nafasi ya ushambuliaji, na wala hajawahi kupewa jukumu la kufunga tangu alipotua Simba SC.

Phiri alisajiliwa Simba SC mwishoni mwa msimu uliopita akitokea ZANACO FC ya nchini kwao Zambia, na ujio wake katika kikosi hicho cha Msimbazi umeanza kuonyesha matunda kufuatia kasi yake ya ufungaji mabao.

Amesema anaamini sana katika kufunga na ndio maana kazi yake imekua rahisi kila anapopata nafasi, lakini kiuhalisia tangu alipoanza kucheza soka nchini Tanzania hakuwahi kucheza kama Mshambuliaji aliyepewa jukumu la kufunga.

Amesema anatamani sana siku moja ama kuanzia sasa akabidhiwe jukumu hilo ili kuendelea kuisaidia Simba SC katika harakati zake za kusaka alama tatu muhimu, kila inapokuwa katika Uwanja wa nyumbani ama ugenini.

“Sijajua mwisho wa msimu kama nitashindanishwa na washambuliaji kwa sababu mimi sichezi nafasi ya ushambuliaji ila nimekuwa natimiza majukumu yangu, nikipata nafasi ya kufunga huwa nafunga”

“Katika majukumu anayonipa mwalimu kufunga ni jukumu langu la ziada, kila wakati huwa namuangalia mtu anaepewa jukumu hilo ambae ni John Bocco kwa michezo ya hivi karibuni”

“Sichukii wakinishindanisha na washambuliaji kama Mayele ila wanachotakiwa kufahamu watu tunacheza nafasi mbili tofauti hivyo mimi sio mshambuliaji.”

“Nimekuwa mfungaji bora kwenye ligi mara kadhaa ila hata huu msimu naweza kuwa mfungaji bora kwa sababu naona naweza kufanya hivyo kwa sababu kumbe wananishindanisha na wafungaji” amesema Moses Phiri

Mshambulaiji huyo alifikisha idadi ya mabao manane ya Ligi Kuu msimu huu, baada ya kuifungia Simba SC mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita mkoani Kilimanjaro katika Uwanja wa Ushirika-Moshi.

PICHA: Young Africans yaifuata Ihefu FC Mbarari
Mshambualiji Coastal Union awaangukia wadau