Mshambuliaji wa Simba SC Mzambia, Moses Phiri ametamba kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos, huku akitamba kuwa Mnyama ataibuka na ushindi na kufuzu Hatua ya Makundi ya mashindano hayo.

Simba SC kesho Jumapili (Oktoba Mosi) watakuwa wenyeji wa Power Dynamos katika mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

Phiri amesema: “Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huu, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, hasa kutokana na ubora wa wapinzani wetu na matokeo ya mchezo wa awali kule Zambia.

“Hivyo kila mchezaji anajua nini wajibu wake na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kwenda hatua ya makundi akili zetu zipo kwenye kuhakikisha tunafanikisha hilo, tupo tayari.”

Simba SC wataingia katika mchezo huo wakiwa na uhitaji wa angalau sare ya bao 1-1 ili kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo, hii ni kufuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2 waliyopata kwenye mchezo wa ugenini Jumamosi (Septemba 16).

SSC Napoli yatoa tamko kwa Victor Osimnhen
Aaron Ramsey aipa ubaridi Wales