Kocha wa Mamelod Sundowns ya Afrika kusini Pitso Mosimane amethibitisha kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo kwa miaka minne.

Mosimane, ambaye alijiunga na ‘The Brazilian’ katikati ya msimu wa 2012/13 ameendelea kuwa kocha bora zaidi nchini Afrika Kusini na kwa Mkataba huo mpya, utamfanya kuwa kocha wa kwanza kudumu kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya Klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari nchini Afrika kusini kocha huyo amesema anajisikia furaha kuwa kwenye familia aipendayo ya Mamelod, huku akiushukuru uongozi wa klabu kwa kuendelea kumwamini.

Pamoja na kumshukuru Rais wa klabu Patrice Motsepe, ametoa shukrani zake kwa wachezaji na benchi zima la ufundi kwa kumuunga mkono klabu hapo.

Tangu kuwasili kwake klabuni Hapo, kukawa mwanzo wa mafanikio akiwaongoza kutwaa Mataji Manne ya Ligi Kuu Afrika Kusini “PSL”, Nafasi ya pili wakimaliza Mara mbili, Ubingwa wa Nedbank Cup, Telkom Cup Mara mbili.

Pia kwa mara ya kwanza aliwaongoza kwenye mafanikio yao ya kwanza Kimataifa ambapo walikuwa Mabingwa wa Afrika mnamo 2016 ukifuatiwa  na Ubingwa wa CAF Super Cup mwaka uliofuatia.

Tamko la Mosimane, limezima kabisa tetesi kuwa angeondoka kwenye klabu hiyo ambayo ataendelea kuitumikia mwisho wa msimu wa 2023/24.

Wanne wamwaga wino Msimbazi
Masumbwi kurejea Julai