Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesema kuna dalili za uwepo wa hujuma zilizopelekea Mahakama ya mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuungua moto na nyaraka zake zote kuteketea.
Mrindoko ameyasema hayo mara baada ya Mahakama hiyo kuungua moto usiku wa kuamkia Mei 19, 2023 na kuongeza kuwa ataunda timu itakayochunguza chanzo cha moto huo ndani ya siku tano, na kisha watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Awali akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Katavi, Regina Kaombwe amesema taarifa za kuungua kwa jengo hilo la Mahakama zilizipatikana majira ya saa sita na robo usiku, kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Shanwe, Mustapha Kimasa.
Amesema, “Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanya juhudi za kuuzima moto uliokuwa tayari umeshasambaa jengo lote la Mahakama na kwamba mlinzi wa Mahakama hakuwepo katika kituo chake cha kazi huku changamoto iliyowakabili ikiwa ni ukosefu wa maji.