Moto ulionza leo Ijumaa Aprili 8, 2022 alfajiri umeteketeza vibanda 36 katika Soko la Kurume lililopo Dar es Salaam baada ya kuunguza sehemu ya soko hilo,na kuunguza maduka ya wafanyabiashara ndogondogo wanaouza mabegi.
Jumapili Januari 16, 2022 Soko la Karume (soko la mchikichini) liliteketea moto na kuharibu mali mbalimbali ikiwamo miundombinu ya umeme.
Kwa mujibu wa naibu katibu wa wafanyabiashara wa soko hilo, Mohamed Sona moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
“Moto umeenza saa 11 alfajiri na vibanda 36 kati ya 96 vimeteketea lakini hakuna madhara kwa binadamu,” amesema Sona
Amesema kuwa moto huo ulidhibitiwa na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala.
Eneo hilo kwa sasa limewekwa uzio huku mafundi kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) wakifanya maandalizi kwa ajili ya kubadilisha nguzo iliyoteketezwa kwa moto katika soko hilo.