Waumini wa kanisa la kwanza la dhehebu ya Baptist nchini Marekani wamebaki na mshangao mkubwa mara baada ya radi kupiga na kuteketeza kanisa lao na mali zenye thamani ya dola milioni 1.
Kanisa hilo ambalo linadaiwa kuwa na miaka 150 tangu lilipojengwa liliteketea Jumanne, Oktoba 23 huku vyombo vyote vilivyomo ndani kuteketea.
Katika kisa cha kushangaza, imebainika kuwa mchoro wa picha ya Yesu uliokuwa kanisani humo haukushikwa na moto hata kidogo.
Waumini wa kanisa hilo ambao walisikitika kwa hasara waliopata kutokana na kisa hicho cha moto walijipa moyo kuona kuwa picha ya Yesu iliyomo ndani haikuguswa na moto.
Katika picha iliyochapiswa kwenye mtandao wa Twitter na Boston Globe, anaonekana akiibeba picha hiyo ya Yesu mkononi.
Akizungumza na jarida la Boston Globe, mshiriki wa kanisa hilo aliyejitambulisha kama Susan Auld alieleza kuwa mchoro huo ungetolewa kwa mmoja wa mapasta aliyehudumu katika kanisa hilo.
Kuhusiana na mkasa huo, pasta wa kwanza wa kanisa hilo Norm Bendroth alisema: ”Imani yetu ni moja. Tunaamini kuwa unaweza kufufuka kutoka kwa majivu, na furaha huja asubuhi,’’ Indaiwa kuwa moto huo ulisasabaisha.