Manchester City wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa West Bromwich Albion mabao 3-2 katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la The Hawthorns.

Mabao ya City yamefungwa na Leroy Sane, Fernandinho pamoja na Raheem Sterling wakati mabao ya West Bromwich Albion yakifungwa na Jay Rodriguez na Matthew Phillips.

Ushindi huo unawafanya Manchester City kuendelea kubaki kileleni mwa Epl wakiwa na pointi 28 baada ya kucheza michezo 10 wakifuatiwa na Man Utd wenye pointi 23.

Katika michezo mingine Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swansea City, babao ya Arsenal yakifungwa na Aaron Ramsey na Sead Kolasinac wakati bao pekee la Swansea likifungwa na Sam Clucas. Liverpool wameichapa Huddersfield Town mabao 3-0.

Crystal Palace wametoka suluhu ya mabao 2-2 na West Ham, mabao a Crytal Palace yamefungwa na Luka Milivojevic kwa njia ya penati pamoja na Wilfried Zaha aliyefunga dakika ya 90 huku mabao ya West Ham yakifungwa na Javier Hernandez pamoja na Andre Ayew.

Yanga, Simba zatoka suluhu huku Kichuya akiweka rekodi ya aina yake
Video: Takwimu za mapato zinazotangazwa na Serikali si sahihi- Zitto Kabwe