Zaidi ya watu arobaini wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa, baada ya moto kutokea katika gereza moja kwenye jimbo la Banten Magharibi mwa Indonesia.
 
Aidha moto huo ambao umezuka alfajiri ya leo Septemba 8, umeteketeza maeneo kadhaa ya jengo la gereza la Tangerang, ambapo baadaye walifanikisha kuuzima.
 
Jengo hilo la gereza limekuwa likihifadhi wafungwa ambao wanatumikia vifungo mbalimbali, kutokana na makosa yanayoambatana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
 
Hata hivyo jengo hilo ambalo lina uwezo wa kuchukua wafungwa 38 limekuwa likichukua wafungwa zaidi ya mara tatu ya uwezo wake, hivyo kusababisha msongamano wa wafungwa.
 
Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu nchini Indonesia imekiri kuwepo kwa msongamano wa wafungwa katika jengo hilo.
 
Sambamba na hayo yote Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha moto huo.

Wizara ya Afya yafanya mabadiliko ya ujenzi
Katibu Mkuu CCM afanya mazungumzo na Zitto Kabwe