Bweni la shule ya mchanganyiko ya St. Mary’s Miambani lililoko Kitui nchini Kenya limeteketea kwa moto mapema leo asubuhi.

Mkuu wa eneo hilo, Muthoka Kilonzo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akielezakuwa bweni husika lilikuwa linabeba wanafunzi 76.

Imeelezwa kuwa wanafunzi pamoja na wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo walifanikiwa kuuzima moto huo, wakitumia michanga na maji.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Citizen TV, hakukuwa na majeruhi walioripotiwa wakati uchunguzi juu ya tukio hilo ukiendelea.

Tukio hilo limeripotiwa ikiwa ni siku chache tu baada ya Waziri wa Elimu, Geore Magoha kuonya dhidi ya vitendo vya wanafunzi wasio na nidhamu kuchoma mabweni kwa makusudi. Hivi karibuni kumekuwa na ripoti ya shule kadhaa za bweni kuteketea kwa moto, matukio ambayo yanaendelea kuchunguzwa.

Molinga akataa kuipa ubingwa Young Africans
Eddie Howe akabidhiwa mikoba Newcastle United