Mabweni ya shule ya African Muslim iliopo wilaya ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro yameteketea kwa moto, leo Agosti 26, na bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa chanzo cha tukio hilo.

Taarifa iliyotolewa shuleni hapo imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea  majira ya saa moja kasorobo, ambapo wanafunzi wote walikua kwenye bwalo la chakula akipata kifungua kinywa.

Hata hivyo taarifa hiyo imeongeza kuwa, moto huo haukuleta madhara kwa mwanafunzi yoyote zaidi ya uharibifu wa vifaa mabwenini. Na hii ni mara ya pili kwa shule hiyo kukumbwa na tukio kama hilo.

Mara ya kwanza tukio la moto lilitokea shuleni hapo na kuteketeza baadhi ya majengo, na hakukuwa na mtu yoyote aliedhurika.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Rajab Kundya amefika shuleni hapo na kutoa pole kwa uongozi na wanafunzi, kwa kuwaambia ni jambo la kumshukuru Mungu, kwani hakuna aliyedhurika.

“Kuthibitisha mapenzi ya mwenyezi mungu kwenu, nimeambiwa hata tukio la awali ya majengo yaliyowahi kuungua na moto, hakuna aliedhurika.

Nimeambiwa kwa kipindi kile nyote mlikuwa sehemu ya ibara (Msikitini), haikutokea nyakati za usikua mbapo wengi wenu mngekua mmelala, ni jambo la kumshukuru sana mungu.” Alisema Alhaji.

Amesema serikali itafanya tathimini ili kujua hasara iliyopatikana na kufanya uchunguzi wa chanzo cha moto huo, ili kufahamu kama yoyote amehusika na tukio hilo.

Rwanda yamsaka ‘mpelelezi wake’ kwa tuhuma za mauaji ya kimbari
Mwinyi ataja sababu za kugombea urais Zanzibar