Watu takribani 15 wamefariki na makumi wamejeruhiwa baada ya moto kuteketeza soko la Gikomba jijini Nairobi nchini Kenya, saa chache zilizopita.
Kwa mujibu wa maafisa wa Serikali pamoja na kitengo cha uokoaji, moto huo ulizuka majira ya saa nane na nusu usiku na kusambaa kwenye majengo kadhaa.
Imeelezwa kuwa ilichukua zaidi ya dakika 90 kuudhibiti moto huo ulioacha janga kubwa la vifo na uharibifu wa mali.
Mratibu wa Mkoa wa Nairobi, Kangethe Thuku amesema kuwa watu 15 wamethibitika kupoteza maisha lakini bado wanaendelea kukagua maeneo ya soko hilo.
“Takriban watu watano walifikishwa hospitalini wakiwa wamekufa tayari lakini bado kuna miili tisa kwenye jengo linaloteketea kwa sababu tunataka kuthibitisha na kuhakikisha usalama upo kwenye majengo,” Thuku anakaririwa na AFP.
- Jose Mourinho kuivurugia Liverpool kwa Nabil Fekir
- Sokratis Papastathopoulos kutua Arsenal wakati wowote
Aliongeza kuwa watu wengine 15 waliokuwa kwenye hali mbaya walikimbizwa kwenye hospitali mbalimbali, lakini watu zaidi ya 70 kwa ujumla walijeruhiwa.
Chanzo halisi cha moto huo bado hakijafahamika au kuwekwa wazi.