Watoto wachanga nane wamepoteza maisha, baada ya moto kuwaka kwenye Wodi la wazazi eneo la Mashariki mwa Aljeria usiku wa kuamkia leo.

Taarifa iliyotolewa na kamanda wa  kikosi cha zimamoto na uokoaji, Nassim Bernaoui, imeeleza kuwa wamefanikiwa kuwaokoa watoto 11, wanawake 107 na wafanyakazi 28, hadi kufikia majira ya saa tisa usiku.

” Tunasikitika na kujutia kuwa tumeshindwa kuokoa maisha ya watoto nane ambao baadhi yao wamekufa kutokana na kuungua moto na wengine wamekufa kutokana na kuvuta moshi mzito” ameongeza Bernaoui.

Amesema kuwa kikosi cha zimamoto kilipeleka watu wakutosha eneo la tukio ambao ndio waliozima moto na kufanya uokoaji japo bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Noureddine Bedoui ameagiza Waziri wa Afya, Mohamed Miraoui, kutembelea hospitalini hapo na kupata taarifa kamili.

Ajali hii ya moto ni ya pili kutokea kwenye wodi la wazazi ndani ya wiki 18 kwenye hospitali hiyo ambayo ni moja kati ya hospitali kubwa tano mjini hapo.

 

 

 

 

Mshtakiwa aomba kujidhamini adai sehemu zake za siri zimetoweka
IGP Sirro awaagiza ma-RPC, OCD kutembelea na kutatua changamoto za wananchi