Wanafunzi kumi wamekufa kwenye ajali ya moto iliyotokea shule ya msingi Islamic (Byamungu) iliyopo kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Rashid Mwaimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kuwa moto ulianza kuchoma bweni majira ya saa tisa usiku kuamkia leo.

Akizungumza na vyombo vya habari, DC Mwaimu amesema kuwa ni bweni la wavulana, watoto wadogo kati miaka 6-13, watoto 6 wamekimbizwa hospitali huku watoto 3 bado hawajajulikana walipo na wanahofiwa kufunikwa na kifusi kwani bweni limeanguka .

Amesema kuwa bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 74.

Suga njia nyeupe kuwa Waziri Mkuu - Japan
Diego Simeone kuikosa Atletico Madrid kwa siku 14

Comments

comments