Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutuma wasaka vipaji wake kumwangalia kiungo wa Benfica ya Ureno, Renato Sanches, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya meneja mtarajiwa, Jose Mourinho.

Kwa mujibu wa gazeti la AS Diario, Juventus ya Italia pia ilikuwa na wasaka vipaji wake wakimmulika kiungo huyo kinda mwenye umri wa miaka 18 aliyekuwa dimbani katika mchezo wa ligi ya nchini Ureno dhidi ya FC Porto mwishoni mwa juma lililopita, ikimtaka kuziba pengo la Paul Pogba anayehusishwa na taarifa za kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Ripoti zinadai kuwa Man Utd wanaweza kuweka mezani ofa ya pauni milioni 30 na nyongeza ya pauni milioni 15 ili kuzikata maini klabu nyingine, ikiwamo Real Madrid.

AS limedai kuwa Real Madrid imemfanya kipaumbele Sanches katika usajili wa kiangazi na Benfica imeripotiwa kuwa tayari kusikiliza ofa ya karibu pauni milioni 46.

 

Juventus Yatangaza Vita Kali Dhidi Ya Arsenal, Man Utd
Waziri Mkuu Ampiga Kijembe Jamal Malinzi