Meneja wa Tottenham Hotspurs Jose Mourinho amejitoa muhanga kwa kuanika hadharani msimamo wa kutokukubaliana na baadhi ya maamuzi yanayotolewa viwanjani kupitia teknolojia ya Video inayomsadia Mwamuzi (VAR).

Mourinho ametangaza dhaharini kupinga baadhi ya matukio yanayoamuliwa na mfumo huo wa kisasa kwa kusema umekua hautoi haki kwa asilimia kubwa huku akiweka bayana mifano ya michezo iliyomalizwa vibaya kwa utata wa VAR.

Amesema michezo dhidi kati ya Liverpool na Everton pamoja na Man City Vs FC Porto iligubikwa na utata mkubwa, kufuatia maamuzi yasiyo ya haki ya VAR.

Mesema mchezo wa Liverpool Vs Everton, dunia ilishuhudia Pickford akicheza rafu mbaya kwa Van Dijk na hakupewa kadi nyekundu. Liverpool walinyimwa goli la ushindi baada ya VAR kuamua Saidio Mane alikuwa amezidi (Offside).

Mchezo kati ya Man City na FC Porto amesema dunia ilishuhudia Ilkay Gundogan akisimama kwenye miguu ya kipa wa FC Porto lakini VAR ikaamuru iwe penalti kwa vijana wa Pep Guardiola na Aguero hakufanya makosa.

“Nadhani mambo mengi yanaelekezwa kwenye uwepo wa VAR. Kabla ya VAR, mambo mengi yalikuwa yanatokea uwanjani, waamuzi nao ni binadamu na walikuwa wanafanya makosa vilevile.”

“Mnanijua kwa miaka mingi, ilikuwa ngumu kwangu kukubaliana na makosa ya kibinadamu lakini nilijufunza, sasa hivi huwa ninakubaliana na makosa ya waamuzi.”

“Tusichokikubali ni makosa ya VAR. Hivyo ninadhani mwamuzi wa ule mchezo (Liverpool vs Everton), tukio lilitokea, mshika kibendera akasema ni ‘Offside’, kila mtu atasema sawa alicheza vibaya lakini ndio imeshatokea.

“Lakini tatizo lilikuwa pale na ni VAR. Sasa hivi kipa wa FC Porto angekuwa amevunjika mguu. Na hakuna anayeelewa kwa namna gani (tunadhani) kuvunjika mguu kwa kipa wa FC Porto kuligeuka kuwa penati dhidi yao.

“Kama ni mwamuzi amefanya kosa, tunaweza kuelewa kutokana na kwamba anakimbia maili 100 kwa saa, lakini ni VAR. Inakuwaje VAR inafanya kosa kama lile? Tukio la Pickford kwangu ni vilevile, ni VAR sio refa.”

Mourinho ataiongoza Tottenham leo usiku kuwavaa Burnley katika dimba la Turf Moor. Huu ni mchezo ambao wataingia wakiwa wanakumbuka sare ya mwisho dhidi ya West Ham United ambapo waliruhusu kufungwa magoli 3 na kupokonywa ushindi.

Mgombea Urais NCCR-Mageuzi aahidi kubadili sheria
Tshishimbi akamilisha AS Vita