Jose Mourinho amesifu kiwango cha mshambuliaji wake Anthony Matrial kwa kusema kuwa mchezaji huyo kwa sasa ana furaha ndani ya klabu ya Manchester United na anacheza kwa kiwango kizuri.

Tayari Martial amefunga mabao manne msimu huu na Mourinho amesema mchezaji huyo anaonekana mwenye furaha siku hizi kwani anacheza vizuri akianza katika kikosi cha kwanza na hata akitokea benchi.

Matrial mwenye umri wa miaka 21 alifanya vizuri katika msimu wa kwanza aliojiunga na Man Utd chini ya kocha Louis van Gaal lakini baada ya ujio wa Mourinho amekuwa hapati nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza kiasi cha kutaka kuondoka katika klabu hiyo.

Kuelekea katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza hapo kesho baina ya Man Utd na Sunderland, Mourinho amesema anafurahi kumuona Matrial akiwa katika hali nzuri kiakili, hari na hata kiwango.

”Nafurahi kumuona akiwa mwenye furaha, mchezo uliopita alicheza vizuri na anaonekana kuwa katika kiwango kizuri” alisema Mourinho.

Kocha huyo ameongeza kuwa kutokuwepo kwa kiungo Paul Pogba sio tatizo kwake kwani kuna viungo wengi wanaoweza kuziba nafasi ya Pogba ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita.

Kesho Manchester United inatarajia kushuka dimbani kukipiga na klabu ya Southampton katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa katika uwanja wa St. Mary’s.

 

Msigwa amvaa Musukuma, amtaka aache kulalamika
Fid Q kuyaanika maisha yake kwenye kitabu, albam