Meneja wa Totenham Hotspurs Jose Mourinho amekiri kufurahishwa na uwezo wa kikosi chake, baada ya kuibuka na ushidni wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya LASK kwenye mcihuano ya Europa League, usiku wa kuamkia leo.
Mourinho amesema sababu kubwa inayompa furaha kupitia kikosi chake ni mabadiliko ya wachezaji aliyoyafanya kwenye mchezo huo, na kumpa matokeo ya ushindi.
Ni wachezaji watatu pekee ambao walibakia kwenye nafasi zao kutoka kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya West Ham United mwishoni mwa juma lililopita.
Wachezaji hao ni Davinson Sanchez, Ben Davies na Sergio Reguilon ambao walikua sehemu ya kikosi kilichocheza jana alhamisi Oktoba 22.
“Nimekifurahia kikosi,” aliiambia BT Sport. “Tunaaminiana hawa wakicheza sana na kuonekana kuchoka tunawaachie wengine wacheze.”
“Kikawaida sikuwahi kufanya kwa mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi hasa tukiwa nyumbani, ni lazima uhakikishe unachukua alama zote tatu, lakini niliwaamini vijana na majibu yalikuwa mazuri, sio mbinu nzuri lakini ni ngumu na salama.” Amesema Mourinho
Mabadiliko hayo ya Mourinho yanamaanisha ana uwezo wa kuwatumia wachezaji kama Son Heung-min, Dele Alli na Giovani Lo Celso katika mzunguko wa pili dhidi ya LASK.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ureno amesema ni vigumu kuwacha wachezaji wenye vipaji vikubwa kama hao nje ya kikosi cha kwanza, lakini kulingana na hali ilivyokuwa msimu uliyopita kwa kuwa na idadi kubwa ya majeruhi, alilazimika kufanya mabadilko.
“Msimu uliyopita nilikuwa na wachezaji wengi wenye matatizo mbalimbali hali iliyopelekea kukosa washambuliaji, kukosa mawinga lakini sasa tuna kikosi kizuri na UEFA kuruhusu kuwa na wachezaji wengi kwenye bench basi nina machaguo mengi.”