Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Pedrito Eliezer Rodríguez Ledesma huenda akaikacha klabu ya Barcelona na kutimkia nchini Uingereza kujiunga na klabu ya Chelsea.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari vya nchini Hispania, Pedro amedhamiria kuondoka nchini Hispania, kutokana na kukabiliwa na mazingira magumu wa kucheza katika kiksoi cha kwanza cha FC Barcelona tangu utawala wa meneja Luis Enrique alipochukua mkondo wake mwaka 2014.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa na dhamira ya kucheza kila juma, lakini kuboreshwa kwa kikosi cha FC Barcelona kwa kusajiliwa kwa Neymar pamoja na Luis Suarez imekuwa sababu kubwa kwake kusubiri katika benchi.

Vyanzo hivyo vya habari vimeendelea kubainisha kwamba mabingwa wa soka nchini Uingereza, Chelsea wanajiandaa kuwasilisha ofa ya Euro milioni 30, ambazo ni sawa na Paund milioni 21.6 ili kukamilisha mpango wa kumsajil Pedro.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Chelsea wamepata nguvu ya kumsajili Pedro baada ya kuzikataa ofa zilizowasilsihwa huko Camp Nou kutoka kwenye klabu kadhaa barani Ulaya kama Arsenal, PSG pamoja na Liverpool.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas, amekua mshawishi mzuri kwa Pedro ili akubali kujiunga nae Stamford Bridge.

Jose Mourinho mara kadhaa amekuwa akiwasiliana na Fabregas, hatua ambayo inachukuliwa kama chagizo la kuongeza ushawishi wa kupatikana kwa mshambuliaji huyo.

Pedro, amekuzwa na kuendezwa na kituo cha FC Barcelona cha La Masia na hakuwahi kucheza klabu nyingine tangu alipoanza kucheza soka la wakubwa.

Roger Federer Ailaumu Mvua
Van Persie atuwa Kwa mbwembwe Istanbul