Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa hatua ya klabu hiyo kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Barani Ulaya katika hatua ya 16 bora si jambo geni kwa klabu hiyo.

Ameyasema hayo mara baada ya Manchester United kucharazwa goli 2-1 na Sevilla katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford, ambapo mabao yote ya klabu hiyo ya Hispania yakifungwa na Wissam Ben Yedder.

“Sijutii matokeo ya kutolewa kwenye michuano hii, Nilifanya kazi kadiri ya uwezo wangu, wachezaji walijitolea pia. Tulijaribu sana, tulishindwa na hiyo ndiyo kawaida ya mchezo huu wa soka.”amesema Mourinho

Aidha, Manchester United walionekana kuzidiwa na klabu hiyo ya Hispania katika mechi zote mbili na ilifungwa kutokana na mfumo wa timu hiyo kucheza kwa kujilinda zaidi kuliko kushambulia.

Hata hivyo, Mourinho amesema kuwa kitendo cha kutolewa kwa Manchester United katika hatua hiyo ya 16 bora si jambo la kushangaa kwani alishawahi kuwaondoa Manchester United katika hatua ya 16 bora wakiwa kwao nyumbani, Old Trafford. akiwa kocha wa Porto (mwaka 2004) na Real Madrid (mwaka 2013).

 

Video: Tsunami nyingine yaikumba Chadema, Polisi yalipua bomu la aliyedai kutekwa
Polisi, Chadema watifuana msibani