Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kumpa heshima mshambuliaji Romelu Lukaku na kuacha kumkosoa.

Mara baada ya mchezo ambao Man Utd waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham mashabiki walimzomea Lukaku kutokana na mchezaji huyo kutofunga goli katika michezo mitano iliyopita ambayo Man Utd imecheza.

Mourinho amesema hakufurahishwa na kitendo cha mashabiki kumzomea Lukaku kwani mchezaji huyo anahitaji kuheshimiwa na anatoa mchango mkubwa uwanjani hata asipofunga goli.

”Mashabiki wananunua tiketi kuingia uwanjani ni haki yao kuonyesha hisia zao lakini kazi yangu ni kuwalinda wachezaji na nafikiri Lukaku ni kati ya wachezaji wanaostahili heshima,” alisema Mourinho.

Kocha huyo ambaye mwanzoni alisema hakuna mchezaji ambaye hatakiwi kukosolewa aliongeza kuwa pamoja nakutofunga magoli Lukaku anacheza vizuri na kutofunga goli katika mechi dhidi ya Tottenham kulitoka na uzuri wa mabeki wa timu hiyo Jan Vertonghen na Eric Dier.

Mdee amnong'oneza Nyalandu kinachoendelea Chadema
LIVE: Rais Magufuli katika mkutano wa hadhara na wananchi Mwanza