Meneja wa klabu ya Tottenham, Jose Mourinho ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa 11 (Novemba) ndani ya Ligi Kuu Nchini England – Jose Amenyakua tuzo hii Baada ya kumaliza Mwezi bila kupoteza mechi yeyote ya Premier League na kuendeleza kuongoza usukani wa ligi hiyo.

Mourinho aliiongoza Spurs kushinda kwa Bao moja Dhidi ya Brighton na West Brom, Kisha kushinda 2-0 Dhidi ya Manchester City na Suluhu mbele ya Chelsea.

Katika tuzo hii amewashinda makocha wenzake, Frank Lampard wa Chelsea, David Moyes wa West Ham na Ole Gunnar Solskjær wa Manchester United.

Wakati huo huo Kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa 11 (Novemba) ndani ya Ligi Kuu Nchini England – Bruno Alifunga Magoli Manne Katika Mechi Nne ndani ya Mwezi huo.

Alifunga Magoli Mawili na Assist Katika Kiwango Bora Cha Mwezi Dhidi ya Eveton, Kisha Alifunga Katika Ushindi Dhidi ya West Brom na Comeback mbele ya Southampton – Amewashinda Wachezaji wenzake, Ben Chilwell wa Chelsea, Jack Grealish wa Aston Villa, Pierre-Emile Hojbjerg wa Tottenham, Angelo Ogbonna wa West Ham na James Ward-Prowse wa Southampton.

Bruno Ambaye amejiunga tu na United January Mwaka huu, Ndiye Mchezaji wa kwanza kubeba tuzo tatu ndani ya Mwaka Mmoja ndani ya PL Tangu Harry Kane alipofanya hivyo Mwaka 2017.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 14, 2020
Kocha Sven aanika mkakati wa kuikabili FC Platnum