Meneja Mpya wa AS Roma ya Italia Jose Mourinho ameanza mbwembwe baada ya kuweka wazi kwamba atapiga panga wachezaji WANANE wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa kuwaacha ama kuwauza kwenye dirisha hili.
Taarifa kutoka Sky Sports Italia zimefichua kwamba Pedro, Justin Kluivert, Steven N’Zonzi na Mlinda Lango Robin Olsen ni miongoni mwa wachezaji wanane ambao wataondoka klabumi hapo.
Mbali ya mastaa hao wachezaji wengine ni Ante Coric, Davide Santon na Federico Fazio.
AS Roma imekuwa ikihusishwa na usajili wa mastaa kibao barani Ulaya ikiwa pamoja na Mlinda Lango wa Wolves Rui Patricio sambamba na kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka ili kuinesha makali kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya Italia.
Msimu uliopita AS Roma ilishika nafasi ya saba kwenye Msimamo wa Ligi ya Italia.
Mourinho amekuwa meneja wa mataji katika kila timu anayoifundisha
isipokuwa Tottenham.