Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich yuko pamoja nae licha ya msimu mbovu wa mabingwa hao wa England.

Chelsea wapo mpaka wapo nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu England baada ya kufungwa Mechi 8 za Ligi kati ya 15 na bado kufuzu kutinga hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ambapo leo Jumatano Desemba 9 wanacheza Mechi ya mwisho ya Kundi lao na FC Porto wakihitaji Sare tu ili kusonga.

Akiongea kuelekea Mechi hii ya UCL, Mourinho, alipoulizwa kama atabakishwa kama Meneja wa Chelsea, alijibu: “Nadhani nimefanya mengi mazuri kwa Klabu hii. Sidhani Mmiliki ni Mtu anaeyumbayumba.”

Mourinho, ambae ni Mreno leo Jumatano anapambana na Klabu ya kwao Ureno FC Porto ambayo aliwahi kuwa Kocha wao, ameeleza: “Abaramovich ameniamini mara mbili.

Huku kukiwa na uvumi kuwa Mourinho atatimuliwa ikiwa atafungwa Mechi mbili mfululizo na Mechi ya leo na FC Porto na kufuatia fuatia kipigo cha Bournemouth, kwenye Mechi ya Ligi Jumamosi iliyopita.

Jumatatu ijayo, Chelsea itacheza na Vinara wa Ligi Leicester City.

Hii ni himaya ya Pili ya Mourinho akiwa na Chelsea baada ya kujiunga nayo tena Mwaka 2013 na kutwaa Ubingwa wa England na Capital One Cup.

Mara ya kwanza kuwa na Chelsea ilikuwa kati ya 2004 na 2007 ambapo alitwaa Ubingwa wa Ligi mara 2 FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.

TP Mazembe Na Etoile du Sahel Kupambana February 2016
Tyson Fury Apokonywa Ubingwa Wa Dunia