Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza, Jose Mourinho amesema alikua pamoja na maamuzi yaliyochukuliwa na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich ya kumuuza mlinda mlango kutoka Jamuhuri Czech, Petr Cech kwa mahasimu wao wa jijini London Arsenal.

Mourinho amejitokeza hadharani na kueleza namna alivyokubaliana na bosi wake katika maamuzi hayo, baada ya kuzungumzwa sana kupitia vyombo vya habari ambapo ilidaiwa alikuwa na msimamo tofauti juu ya Cech kusajiliwa na Arsenal.

Meneja huyo kutoka Ureno amesema ameshangazwa sana na maeleozo ambayo yamekua yakitolewa dhidi yake, lakini ukweli ni kwamba hakupinga hata kidogo mipango ya mlinda mlango huyo kuondoka klabuni hapo na kuelekea upande wa pili wa jiji la London.

Amesema lengo lake lilikua ni kuendelea kubaki na Cech baada ya kumshuhudia akiitumikia The Blues kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita huku yeye akiwa chanzo cha ujio wa mlinda mlango huyo klabuni hapo.
Amesema ni vigumu kuwazuia watu kusema ama kuandika chochote kinachomuhusu hasa katika kipindi hiki cha usajili ambapo mambo mengi huchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari.

Jose Mourinho, alidaiwa kuwa na msimamo tofauti na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich kwa kutaka Petr Cech auzwe nje ya England kwa kuhofia kuwapa silaha wapinzani wake, lakini msimamo wa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 33 ulipingana nae, baada ya kuweka wazi anahitaji kubaki jijini London.

Abramovich aliingilia kati mzozo uliokua ukiendelea baina ya Mourinho dhidi ya Cech kwa kuamuru mchezaji huyo kupewa uhuru wa kujiunga na klabu anayoitaka jijini London, huku tayari klabu ya Arsenal ikiwa imeshaonyesha nia ya kumsajili.

Then Gunners walikamilisha mpango wa kumsajili Petr Cech mwanzoni mwa juma hili, kwa ada ya uhamisho wa paund million 10.

Ngoja Ngoja Za Man Utd, Arsenal Zawapa Nafasi BVB
Uvumilivu Wamshinda Mancini, Amruhusu Shaqiri Kuondoka