Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ kutoka nchini Ufaransa, Moussa Diaby kutoka Bayer Leverkusen kwa ada iliyovunja Rekodi ya klabu.

Miamba wa Saudi Arabia Al Nassr pia walivutiwa na Diaby na wakaingia kwenye vita vya kutaka kumgombea na Villa, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alikataa kuhamia Mashariki ya Kati ili kuungana na Unai Emery katika Villa Park.

Mkataba huo sasa umekamilika na tayari Diaby amesafiri kwenda Marekani kuungana na timu yake mpya kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Villa wanadaiwa kutenga zaidi ya pauni milioni 50 ili kumsajili Diaby, ambaye anakuwa rekodi mpya ya usajili wa Villa.

Diaby anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Villa msimu huu wa majira ya joto, kiungo Youri Tielemans na beki wa kati Pau Torres, kuhamia West Midlands.

Diaby ambaye ni winga wa kulia kwa asili, alifurahia msimu mzuri zaidi wa kazi yake mwaka jana Jumapili (Julai 23).

Kwenye mechi 48 katika michuano yote, Mfaransa huyo alipachika mabao 14 na kutoa ‘asisti’ za mabao 11.

Kutakuwa na muunganiko pale Villa Park kwa Diaby na winga mwenzake Leon Bailey, ambaye aliondoka Leverkusen miaka ishirini iliyopita.

Chama atuma salamu Ligi Kuu, Kimataifa
Nickson Kibabage: Mashabiki wasiwe na wasiwasi