Klabu ya West Ham imemteua David Moyes kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Slaven Bilic ambaye ametimuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Moyes mwenye umri wa miaka 54 amepewa mkataba wa miezi 6 na atawatumikia wagonga nyundo hao wa London mpaka ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo wa zamani wa klabu za Everton na Manchester United hakuwa na kazi ya ukocha tangu mwezi Mei wakati alipojiuzulu kuifundisha klabu ya Sunderland baada ya klabu hiyo kushushwa daraja.

Mwenyekiti msaidizi wa West Ham David Sullivan amesema klabu hiyo ilihitaji kuwa na mtu mwenye uzoefu ,utambuzi wa ligi ya Uingereza na wachezaji wake na wanaamini kwamba David Moyes anaweza kuwaimarisha wachezaji.

Tangu alipoodoka katika klabu ya Everton aliyoitumikia kwa miaka 12 bila kushinda taji lolote David Moyes amekuwa kocha ambaye anafukuzwa katika kila timu anayokwenda kwa kuwa haonyeshi maendeleo na mafanikio makubwa katika timu hizo.

Mchezo wa kwanza ya Moyes itakuwa dhidi ya Watford katika ligi ya Uingereza mnamo mwezi Novemba 19.

Safari ya Said Ndemla yasogezwa mbele
Miaka miwili ya JPM yaimarisha huduma Muhimbili