Msanii wa bongo Movie na mpenzi wa Moses Iyobo, Aunty Ezekiel ni moja kati ya wasanii ambao kwa kiasi kikubwa mahusiano na familia ni vitu ambavyo vimebadilisha mwenendo wa maisha yake.

Ifike wakati wasanii wakike wajitambua, wajiheshimu na wajijali, kuwa msanii haimanishi kufanya mambo yasiyo na maadili katika jamii, kuna namna nyingi ya kutengeneza stori na watu wakakusikia na jina lako likabakia midomoni mwa watu, si kama ambavyo wasanii kama kina Gigy Money wanachofanya kwenye mitandao ya kijamii.

Anty Ezekiel ni moja ya wasichana waliowahi kusumbua sana miaka ya nyuma, ni moja ya watu waliokuwa hawaishiwi mikasa na stori zisizo na maadili katika jamii.

Mara tu baada ya kuingia katika dimbwi la mapenzi na mcheza shoo, Moses Iyobo maisha yalianza kumbadilikia na yamekuja kumbadilika zaidi baada ya wawili hao kujipatia zawadi ya kabinti kao ka kwanza Cookie.

Siri kubwa ambayo Aunty Ezekiel ameweza kufaulu na wanawake wengi hufeli ni kwamba Aunty Ezekiel ameweza kuiishi sheria ya kupunguza marafiki wasio na tija katika maisha yake lakini kubwa kuliko yote Aunty ameweza kuishi akiamini kile anachofikiria yeye, amekuwa si mtu wa kusikiliza maneno ya watu ambayo hulenga kubomoa kitu fulani.

Kwa mtazamo wa nje naweza sema baba Cookie amefanya kazi kubwa kumuweka Aunty kwenye mstari, na kumfanya kuwa mwanamke anayejiheshimu, Anty Ezekiel wa sasa si Yule wa kipindi kile.

Aunty awe mfano kwa wanawake wengine wa bongo movie hata bongo fleva, wengine hutengeneza skendo wakisingizia kazi ndio zinawaingiza katika majanga hayo.

Itambulike kuwa umri unaenda, na kila kitu kina mwishio hizo drama wanazocheza zitakwisha na watajikuta wamekosa kila kitu.

Juan Mata akataa kiasi hiki cha fedha kwenda China
Ngemela akiri CCM kuyumba uchaguzi mkuu 2015