Bashir Fenel, mmoja kati ya wapambe wa karibu wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuchakachua uraia wake.

Bashir alikuwa akionekana mstari wa mbele katika mikutano ya kampeni ya Lowassa na anasadikika kuwa moja kati ya watu waliounda kamati ya ushindi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa nyaraka za uraia alizokutwa nazo baada ya kukamatwa zilionesha utata wa utambulisho halisi wa utaifa wake.

Edward Lowassa akisalimiana na Bashir Fenel, wakati alipokuwa CCM

Edward Lowassa akisalimiana na Bashir Fenel, wakati alipokuwa CCM

Kamanda Kova alieleza kuwa kupitia cheti cha kuzaliwa alichokutwa nacho, Fenel alionekana kuwa alizaliwa Julai 11,1969 mjini Dodoma huku Hati yake ya kusafiria ikionesha kuwa alizaliwa Nairobi, Kenya siku hiyohiyo (Julai 11, 1969).

“Hizi taarifa zimetuchanganya sisi kiasi kwamba tunashirikiana na idara ya Uhamiaji katika kumhoji mtuhumiwa kwa sababu kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Uhamiaji,” alisema Kamanda Kova.

Bashir alikamatwa na jeshi la polisi Novemba 9 mwaka huu katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.

"TSHABALALA" Mchezaji Bora Mwezi Oktoba
Raheem Sterling: Sijutii Kuondoka Liverpool